Ratiba Ligi kuu NBC Leo 10/2/2025, Ratiba Ligi kuu NBC Leo 10 February 2025, Ratiba Ligi kuu NBC Leo 10 Februari 2025, Ratiba Ligi kuu ya Tanzania NBC Leo 10/2/2025
Ratiba Ligi kuu NBC Leo 10/2/2025
Ligi kuu ya Tanzania NBC Itaendelea leo 10/2/2025 kwa mechi tatu kuchezwa , Katika makala hii Ligikuuforum tunaangazia mechi hizo
Kengold vs Fountain Gate
Katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kutakuwa na mchezo wa Ligi kuu NBC kati ya wenyeji Kengold watakaokuwa nyumbani kucheza dhidi ya Fountain Gate kutoka katika mkoa wa Manyara, Ikumbukwe Fountain Gate wametoka kutoa sare na Simba , wakati Kengold wao waliweza kuchezea Kichapo cha bao 6 kwa 1 kutoka kwa Yanga, Mechi hii ya Kengold vs Fountain Gate itaanza mapema saa nane mchana.
KMC vs Singida Black Stars
Katika uwanja wa KMC kutakuwa na mchezo mwingine wa Ligi kuu NBC Kati ya KMC wenyeji watakaowakaribisha Singida Black Stars kutoka Singida, KMC wametoka kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Azam kwa bao 2 kwa 0, wakati Singida Black Stars wao wametoka kutoa sare mechi yao ya mwisho walipocheza na Kagera Sugar , mechi ilimalizika kwa sare ya 2 kwa 2. Mechi ya KMC vs Singida Black Stars leo 10 February 2025 itaanza saa kumi na Robo.
JKT Tanzania vs Yanga
Maeneo ya Mbweni Jijini Dar Es Salaam kutakuwa na mchezo kati ya JKT Tanzania dhidi ya Mabingwa na vinara wa ligi kuu NBC Klabu ya Yanga mechi ikipangwa kuchezwa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mechi kati ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania itaanza saa kumi na robo kwa saa za AFRIKA Mashariki, JKT Tanzania wanaingia katika mchezo huo wakiwa wametoka kupoteza mbele ya Coastal Union kwa bao 2 kwa 1 huku Yanga wao wakiwa wametoka kushinda bao 6 kwa 1.
Soma Pia
- Msimamo ligi kuu ya Wanawake Tanzania 2024-2025
- Matokeo Ya Yanga vs Copco leo 25 January 2025
- Msimamo Ligi daraja la Kwanza Tanzania 2024-2025
- Ratiba ya Azam Ligi kuu 2024-2025 Raundi ya Pili
- Ratiba ya Simba Raundi ya Pili Ligi Kuu 2024-2025
- Ratiba Ya Yanga Raundi ya Pili Ligi kuu 2024-2025
- Ratiba Ya Raundi ya Pili Ligi kuu 2024-2025
- Ratiba Mpya Ligi kuu NBC 2024-2025 Raundi ya Pili
Leave a Reply