Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21/2/2025

Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21/2/2025
Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21/2/2025

Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21/2/2025, Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21 February 2025, Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21 Februari 2025

Ratiba Ligi kuu NBC Leo 21/2/2025

Ligi kuu ya Tanzania Bara NBC inaendelea leo kwa mechi mbili kuchezwa katika viwanja viwili tofauti mechi ya Kwanza ikichezwa saa nane na mechi nyingine ikichezwa saa kumi na robo kwa saa za Afrika Mashariki

 

Tanzania Prisons vs Tabora United leo 21/2/2025

Mechi hii ni mechi ya mapema kwa leo ikichezwa saa nane kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki , Mechi hii Itachezwa katika uwanja wa Wa Sokoine jijini Mbeya.

 

Mpaka sasa Tanzania Prisons wapo katika nafasi ya 14 KATIKA ligi yenye timu 16 ikiwa na Jumla ya Points 17, wakati Tabora United wao wapo katika nafasi ya tano na Points zao 33. Tabora United wao wanatafuta kuwa ndani ya timu nne za Juu yani Top 4 wakati Tanzania Prisons wao wanapambana kutoka katika nafasi za chini kwenye msimamo.

JKT Tanzania vs Kagera Sugar leo 21/2/2025

Timu ya JKT Tanzania maarufu kama wazee wa Kichapo cha Kizalendo leo 21 February 2025 watakuwa katika uwanja wao wa Nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni wilaya ya Kinondoni kuwakaribisha timu ambayo makao yake makuu ni wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

 

Mechi ya JKT Tanzania vs Kagera Sugar 21 Februari 2025 itachezwa kuanzia saa kumi na Robo kwa saa za Afrika Mashariki.

Mpaka sasa JKT Tanzania wapo katika nafasi ya 8 wakiwa na points 23 wakati klabu ya Kagera Sugar bado iko nafasi za Chini nafasi ya 15 kati ya timu 16 ikiwa na Points 15.

 

Katika mechi ya Raundi ya Kwanza Ligi kuu NBC mechi kati ya JKT Tanzania vs Kagera Sugar ilimalizika kwa sare ya bila mabao yani Kagera Sugar 0 – 0 JKT Tanzania